TETESI ZA SOKA ULAYA WIKI HII - MALIKITA SAFARI FITNESS

Recent Posts

test

Monday 16 April 2018

TETESI ZA SOKA ULAYA WIKI HII



Thomas Lemar
Thomas Lema

Image
caponaco yaangalia kumchukua kiungo kutoka Ufaransa Thomas Lemar msimu wa majira ya joto. Timu za Arsenal na Liverpool pia zimeonekana kumtupia jicho Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22.(Telefoot)
Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic anasema ananafasi kubwa ya kuchezea timu ya Sweden katika michezo ya kombe la dunia nchini Urusi,licha ya kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amestaafu kucheza soka ya kimataifa tangu 2016 (Sun)


Aberdeen manager Derek McInnes
Derek McInnes
Image caption
Aliyekuwa mchezaji wa West Brom,Derek McInnes na mkuu wake wa Baggies Tony Mowbray ni miongoni mwa waliopendelewa kupata kazi ya kuwa meneja wa West Brom (Mirror)
Rais wa Roma James Pallotta anasema klabu hio 'haina nia ya kumuuza' mlinda mlango kutoka Brazil Alisson(25), ambaye ana aminiwa kuhamia Liverpool.
Mlinzi wa Chelsea Antonia Rudiger,25, anasema hajajua sababu ya yeye kutocheza dhidi ya Southampton, akiongezea kuwa alikuwa 'tayari kabisa' kwa ajili ya mechi ya Jumamosi


Newcastle goalkeeper Martin Dubravka catches the ball
Dubravka
Haki miliki ya picha
Image caption

Newcastle wanajipanga kumsajili mlinda mlango Martin Dubravka kwa mkataba endelevu. Mslovak huyo,29, aliungana na Magpies kwa kukopeshwa na timu ya Sparta Prague mwezi Januari. (Express)
Mkuu wa Newcastle Rafael Benitez anatarajia kufanya mazungumzo na mmiliki wa timu, Mike Ashley kabla ya kusaini mkataba mpya . Benitez anataka kuhakikisha kuwa kuna fedha za kutosha za kufanyia usajili wa wachezaji katika msimu wa majira ya joto kabla ya kuingia katika klabu hio.(Telegraph)


Wilfried Zaha
WILFRED ZAHA
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema anajutia kwamba hakuweza kumshawishi winga wa Eagles Wilfried Zaha (25) kuchezea timu ya England dhidi ya Ivory Coast. (Mail)
Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham wanampango wa kurejea juhudi za kupata fedha zaidi kutoka kwa marupurupu wanaolipia nchi za nje kutangaza mechi za Premier League. (Mail)
Mshambuliaji wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 25, anasema kushinda Champions League ni muhimu zaidi kuliko yeye kuwa mfunga goli bora zaidi wa Premier League na kupata tuzo ya Golden Boot. (Guardian)
Credit: BBC