UMUHIMU
WA MAZOEZI KWA VIUMBE HAI WOTE
Mazoezi ni
muhimu saana kwa viumbe hai wote.
na wote hua tunafanya mazoezi kulingana na hali na mazingira.wanyama kwa kua
hawajapewa akili hua wanafanya mazoezi pasipo kujua kama wanafanya mazoezi au
la . vivyo hivyo hata sisi wanadamu kuna kipindi tunafanya mazoezi pasipo kujua
kama tuna fanafanya mazoezi
.na hicho kipindi ni pale tunapokua watoto kwani
mungu ametutengenezea mazingira ambayo kipindi hicho kila mmoja lazima apitie
kwenye michezo mingi na kukimbia bila sababu. tunapokua na akili yaani umri wa
kujitambua ndio tunaamrishwa na kuambiwa umuhimu wa mazoezi. Kwani jambo hili
japo somo lake linafundishwa kuanzia
shule za awali yaani chekechea kuhusu umuhimu wa mazoezi lakini jamii bado ni
wagumu kukubaliana na elimu hiyo au kutekeleza .lakini kutokukubali kwao
haimaanishi kua hayatokei madhara yatokanayo na kukataa kwao.la hasha madhara
yake ni makubwa na yanatia simanzi kwa kiwango kikubwa sana. kwani wataalam wa
afya wanasema 27% ya vifo vinavyotokea
hasa nchini kwetu ni vifo vinavyoweza kuepukika endapo tu watu
watabadili tabia ya kupenda kufanya mazoezi .wewe mwananchi serikali yetu kupitia kwa mama yetu mpendwa makamu wa raisi
mama samia suluh imegundua kua watu wake wanaelekea kwenye shimo. ikapelekea kuzindua siku maaalumu kwa
ajili ya watu wote wafanye mazoezi .serikali ilizindua siku hiyo ili kukumbusha
uwe na utamaduni wa kufanya mazoezi kwa faida ya kwako na jamii iliokuzunguka
lakini cha ajabu watu wengi uzinduzi huu wanafananisha na uzinduzi wa barabara
au uzinduzi mwingine kwani kiukweli bado watu hawajazinduka kabisa
.unapomuambia mtu kuhusu mazoezi analeta visingizio vingi lakini sababu zote
hizo hazina mashiko .kumbuka uzinduzi huu ni kuzindua akili yako ushike njia
sahihi ya afya mwenye jukumu la kutunza afya ni jukumu la kila mtu mwenyewe
binafsi wala sio jukumu la mama samia suluh wala sio la rais wetu
magufuli.hakika kuumbwa kwetu hapa duniani ni kwa ajili ya kumtumikia mwenyezi
mungu maana ya kumtumikia ni kufuata maagizo yake kwa hiyo mazoezi pia ni
sehemu ya maagizo kwetu kutoka kwake kwani .mwili usipofanya mazoezi ni sawa na
chuma kukaa bila kutumika lazime kishike kutu na kupelekea kuzeeka .hivyo
ukishiriki mazoezi unategemea kupata faida mbili kwa wakati mmoja kwanza
utapata Baraka kwa sababu umetekeleza
kanuni alizotuwekea .na faida ya pili utaboresha afya yako.pia usipofanya
mazoezi unapata hasara mbili kwa wakati mmoja kwanza utapata dhambi kwa kua umekataa
maamrisho ya mwenyezi mungu pia utapata afya mbovu na ukipoteza maisha chanzo
chake kikibainika kwa sababu ya kutofanya mazoezi bila shaka hautakua tofauti
na mtu aliepoteza maisha kwa kujinyonga kwani Yule aliejinyonga kwa kamba
katumia maamuzi ya ghafla lakini mtu aliekufa kwa maradhi nyemelezi amejinyonga
taratibu kwa muda mrefu.kwa hiyo acha kufuata kamba utakayotumia kujinyonga kwa
kufuata njia sahihi ya afya NAMALIZIA KUSEMA ZINDUKA……ZINDUKA……ZINDUKA…….MAMA
SAMIA SULUH AMEKUZINDUA