MALIKITA SAFARI FITNESS

Recent Posts

test

Breaking

Monday 16 April 2018

TETESI ZA SOKA ULAYA WIKI HII

April 16, 2018
TETESI ZA SOKA ULAYA WIKI HII



Thomas Lemar
Thomas Lema

Image
caponaco yaangalia kumchukua kiungo kutoka Ufaransa Thomas Lemar msimu wa majira ya joto. Timu za Arsenal na Liverpool pia zimeonekana kumtupia jicho Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 22.(Telefoot)
Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic anasema ananafasi kubwa ya kuchezea timu ya Sweden katika michezo ya kombe la dunia nchini Urusi,licha ya kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amestaafu kucheza soka ya kimataifa tangu 2016 (Sun)


Aberdeen manager Derek McInnes
Derek McInnes
Image caption
Aliyekuwa mchezaji wa West Brom,Derek McInnes na mkuu wake wa Baggies Tony Mowbray ni miongoni mwa waliopendelewa kupata kazi ya kuwa meneja wa West Brom (Mirror)
Rais wa Roma James Pallotta anasema klabu hio 'haina nia ya kumuuza' mlinda mlango kutoka Brazil Alisson(25), ambaye ana aminiwa kuhamia Liverpool.
Mlinzi wa Chelsea Antonia Rudiger,25, anasema hajajua sababu ya yeye kutocheza dhidi ya Southampton, akiongezea kuwa alikuwa 'tayari kabisa' kwa ajili ya mechi ya Jumamosi


Newcastle goalkeeper Martin Dubravka catches the ball
Dubravka
Haki miliki ya picha
Image caption

Newcastle wanajipanga kumsajili mlinda mlango Martin Dubravka kwa mkataba endelevu. Mslovak huyo,29, aliungana na Magpies kwa kukopeshwa na timu ya Sparta Prague mwezi Januari. (Express)
Mkuu wa Newcastle Rafael Benitez anatarajia kufanya mazungumzo na mmiliki wa timu, Mike Ashley kabla ya kusaini mkataba mpya . Benitez anataka kuhakikisha kuwa kuna fedha za kutosha za kufanyia usajili wa wachezaji katika msimu wa majira ya joto kabla ya kuingia katika klabu hio.(Telegraph)


Wilfried Zaha
WILFRED ZAHA
Meneja wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema anajutia kwamba hakuweza kumshawishi winga wa Eagles Wilfried Zaha (25) kuchezea timu ya England dhidi ya Ivory Coast. (Mail)
Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham wanampango wa kurejea juhudi za kupata fedha zaidi kutoka kwa marupurupu wanaolipia nchi za nje kutangaza mechi za Premier League. (Mail)
Mshambuliaji wa Liverpool kutoka Misri Mohamed Salah, 25, anasema kushinda Champions League ni muhimu zaidi kuliko yeye kuwa mfunga goli bora zaidi wa Premier League na kupata tuzo ya Golden Boot. (Guardian)
Credit: BBC

Tuesday 10 April 2018

Manchester City wataweza kulipa kisasi kwa Liverpool UEFA leo?

April 10, 2018
Manchester City wataweza kulipa kisasi kwa Liverpool UEFA leo?

Ni katika mchezo wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya ambapo kwa hakika Man City wana kibarua kizito sana kwani wanatakiwa kuifunga Liverpool bao 4-0 maana mechi iliyopita, Man City walibamizwa 3-0 pale Anfield mjini Liverpool.
Wachezaji wa Timu ya Man City wakishangilia goli lililofungwa na Mchezaji Sergio Kun Aguero hivi karibuni.
Kiungo wa City, Fernandinho mwenye umri wa miaka 32 anasema lile juma gumu lililowakabili la kuchapwa kila walikoenda sasa limeisha na ni wakati sasa wa wachezaji wazoefu kuchukua nafasi yao na kuliongoza Jahazi.
Tangu Man City walipopoteza pale Anfield jumatano, pia katika ligi walichapwa 3-2 na Manchester United.
Liverpool ilifunga mara tatu ndani ya dakika 19 za kipindi cha kwanza katika mzunguko wa kwanza.
Ikiwa upande wa Jurgen Klopp utaweza kushinda katika Uwanja wa Etihad, City watalazimika kushinda angalau mara tano ili kuendelea kufikia nafasi ya nne.
Ni Timu mbili pekee katika historia ya Champions League ambazo zimewahi kujikwamua kutoka katika deni la magoli matatu au Zaidi katika kipindi cha mtoano. Sawa na deni analokabiliana nalo Man City.
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia mojawapo ya magoli waliyoyafunga msimu huu, 2018
Deportivo La Coruna ikiwa nyuma ya AC Milan 4-1 mwaka 2004 walifanikiwa kupindua matokeo kwa 4-0 in katika mechi ya marudiano.
Katika siku za hivi karibuni, ni Barcelona iliyobadilisha matokeo ya 4-0 dhidi ya Paris St-Germain kwa kushinda 6-1 katika mechi ya marudio uwanja wa Noe Camp msimu uliopita.
Katika mchezo mwingine wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya, Roma itashuhudiwa wakikwaana na Barcelona katika uwanja wa Stadio Olimpico.
Nyota wa klabu ya soka ya Barcelona Luis Suarez, Lionel Messi na Moussa Dembele wakishangilia goli waliloifungia klabu hiyo hivi karibuni.
Meneja wa Roma Eusebio di Francesco amekiri kwamba kwa hakika kukutana na Barcelona anakutana na alichokiita Mashine lakini anabaki na matumaini makubwa.
Waitaliano hao wanakutana na Wahispania huku waitaliano wakiwa na hasira za kuchapwa bao 4-1 katika mzunguko wa kwanza.
Pia Roma walichapwa 2-0 na Fiorentina aliyeko nafasi ya saba na sasa wana point 21 nyuma ya viongozi wa Seria A Juventus
Wachezaji wa AS Roma kwenye moja ya michezo yao ya hivi karibuni kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya, 2018
Katika hali ya tofauti, Barcelona wakiwa na Lionell Messi wako pointi 11 juu na bado Meneja wao Ernesto Valverde pamoja na kuwa watakuja na faida ya magoli matatu kibindoni bado amesema mechi hii dhidi ya Roma hawataichukulia kawaida na kwa hakika wataingia Uwanjani kama vile matokeo ni 0-0.
Katika upande wa Championship Cardiff City wataondoka katika nafasi ya pili kama watashindwa kuwapiga Aston Villa na iwapo pia Fulham itawachapa Reading wanaopambana kujiokoa kushuka daraja.
Source: BBC



Tuesday 27 February 2018

SHIRIKI MAZOEZI MARA KWA MARA UEPUKE KUJICHUKIA NA UPUNGUZE GHARAMA YA KUTAFUTA UREMBO.

February 27, 2018
SHIRIKI MAZOEZI MARA KWA MARA UEPUKE  KUJICHUKIA NA UPUNGUZE GHARAMA YA KUTAFUTA UREMBO.


Leo tutazungumzia kuhusu urembo au muonekano(shape)
Kila mtu anapenda aonekane mzuri machoni mwa jamii iliomzunguka.uzuri ni maana pana au ina mambo mengi sana  ila nitaelezea kwa uchache tu kama vile uzuri wa ngozi na muonekano wa umbo (shape).Bila shaka unaweza kua shahidi kwa namna moja ama nyingine tunashudia serikali yetu pendwa  ikitumia nguvu kubwa kukataza na kupiga vita wananchi wake wasitumie vipodozi  na madawa mengine yenye viambata vyenye sumu kwa lengo la kutaka urembo.ila kwa bahati mbaya pamoja na kutumia nguvu kubwa lakini bado wananchi walengwa hawaoni au kutii amri ya serikali kuacha kutumia bidhaa hizo.japo serikali imewalenga zaidi wafanya biashara wanaouza bidhaa hizo.wakati walengwa wakiendelea kutafuta bidhaa hizo kwa hali na gharama yeyote ile ili watumiekama nilivyosema kila mmoja  anatamani urembo kwa hiyo watu walio wengi  wanapenda matokeo ya haraka bila kujali kama njia wanayoitumia ni sahihi au la.kwa kifupi watu wanapenda kutumia njia  ya mkato.mwenyezi mungu ametuumba tofauti tofauti kwa maksudi yake wala hajafanya makosa katika hilo.ninamaanisha kuwa kuna wanene,wembamba,wafupi,warefu,weupe,weusi,maji ya kunde nk.sawa na hali nilizorodhesha hapo juu kila mmoja ajijue yupo kwenye kundi gani. hatmae usimame kwenye kioo na ujiangalie hatmae umshukuru sana mwenyezi mungu na kumpa sifa lukuki kwa kukuumba  hivyo ulivyo  ikiwezekana piga na vigele gele kuonyesha furaha yako. Kwani wewe hivyo ulivyo ni mrembo na mzuri endapo tu utafuata njia sahihi na salama .ila kinyume chake watu walio wengi wanajichukia na kutokujikubali kujiona hivyo walivyo na kutamani shape na rangi ya watu wengine. na kupelekea kutumia gharama kubwa kwa kununua  vipodozi au madawa yenye viambata vyenye sumu na kuharibu afya zao.mwili wa mwanadamu sio sawa na chuma unataratibu zake namna ya kuufanya uwe na muonekano mzuri kuanzia (shape)umbo,ngozi .nk .chuma unaweza ukakiokota vichakani ukaamua kionekane kipya kwa kupaka rangi .wakati mwili ili ngozi ionekane vizuri inanzia ndani ya mwili hadi nje ya mwili walio wengi wanakazania  muonekano wa nje tu bila kuanzia ndani .njia ya kua na muonekano mzuri ni rahisi sana wala haina gharama ni kufanya mazoezi ya viungo tu.kwani unapofanya mazoezi faida yake ni kubwa  na nyingi japo leo tunazungumzia kuhusu urembo tu.
MAZOEZI YANA FANYAJE KAZI KWENYE UREMBO WA NGOZI?
Mazoezi yanasaidia sana kwenye urembo wa ngozi .kwani unapofanya mazoezi  na kutoa jasho inafungua vinyweleo au vitundu vidogo vilivyo kwenye ngozi na kupelekea kusaidia ngozi kua katika muonekano mzuri,sababu ya pili utahitaji kunywa maji mengi  kwani unaposhiriki mazoezi hupelekea kua na uhitaji mkubwa wa maji (KIU)na unapokunywa maji mengi inasaidia kua na afya ya ngozi,sababu ya tatu ni kwamba mwenyezi mungu ametupatia aina nyingi ya chakula na kila chakula kina fanya kazi yake katika mwili wa mwanadamu .unapofanya mazoezi husaidia kuharakisha mwendo wa chakula ambacho kimepangwa kifanye kazi katika eneo la ngozi.sababu zipo nyingi ila kwa hizo chache nilizozitaja inaonyesha picha kiasi gani umuhimu wa mazoezi kwa watu wote wanawake kwa wanaume
MAZOEZI YANAFANYAJE KAZI KUTENGENEZA  UMBO(SHAPE)
Mazoezi yanafanya kazi moja ambayo naweza kuiiita ya ajabu sana.kwani yanaongeza mwili lakini pia yanapunguza mwili kwa wakati mmoja kutegemeana na mtu alivyo yaani ni mnene au mwembamba.kwa kifupi yanamuacha mtu asili alionayo
Mfano;kama mtu asili yake ni mnene alafu hafanyi mazoezi  atakua mnene zaidi .akishiriki mazoezi mara kwa mara itapunguza ziada aliyonayo atabaki na unene wa asili yake na kupelekea kua mwepesi na ukakamavu na kuongeza nguvu nk.hivyo hawezi kujichukia mwenyewe kwani  sisi wote ni  mashahidi  mtu akiwa mnene hua anaitwa majina mengi yenye kuudhi na yasiofaa kama vile huitwa  minyama uzembe,bonge,na mengi mengineyo yasiyofaa kuandikwa .kwa hiyo majina ya hovyo anayoitwa ukijumlisha na udhaifu alionao hupelekea kujichukia na kutamani umbo la mtu  mwingine na kulaani alivyo
Mfano mwingine;kama mtu ni mwembamba halafu hauna kawaida ya kushiriki mazoezi unakua mwembamba zaidi .ukishiriki mazoezi mara kwa mara unaongezeka mwili(unene) japo huwezi kunenepa kufikia hatua ya kuonekana bonge. Kwa hiyo hutoitwa tena majina ya hovyo na ya kuudhi kama vile mchongoma,kimbaumbau nk.na kupelekea kuijichukia na kulaani umbile ulilonalo .fanya mazoezi uwe na umbo (SHAPE) ya kuvutia  pia upate na faida zingine za afya.ZINDUKA…..ZINDUKA…..ZINDUKA…… MAMA SAMIA SULUHU  AMEKUZINDUA

Wednesday 7 February 2018

NEWS

February 07, 2018
NEWS

UMUHIMU WA MAZOEZI

February 07, 2018
UMUHIMU WA MAZOEZI
                                      UMUHIMU WA MAZOEZI KWA VIUMBE HAI WOTE

Mazoezi ni  muhimu  saana kwa viumbe hai wote. na wote hua tunafanya mazoezi kulingana na hali na mazingira.wanyama kwa kua hawajapewa akili hua wanafanya mazoezi pasipo kujua kama wanafanya mazoezi au la . vivyo hivyo hata sisi wanadamu kuna kipindi tunafanya mazoezi pasipo kujua kama tuna fanafanya mazoezi 







.na hicho kipindi ni pale tunapokua watoto kwani mungu ametutengenezea mazingira ambayo kipindi hicho kila mmoja lazima apitie kwenye michezo mingi na kukimbia bila sababu. tunapokua na akili yaani umri wa kujitambua ndio tunaamrishwa na kuambiwa umuhimu wa mazoezi. Kwani jambo hili japo somo lake  linafundishwa kuanzia shule za awali yaani chekechea kuhusu umuhimu wa mazoezi lakini jamii bado ni wagumu kukubaliana na elimu hiyo au kutekeleza .lakini kutokukubali kwao haimaanishi kua hayatokei madhara yatokanayo na kukataa kwao.la hasha madhara yake ni makubwa na yanatia simanzi kwa kiwango kikubwa sana. kwani wataalam wa afya wanasema 27% ya vifo vinavyotokea  hasa nchini kwetu ni vifo vinavyoweza kuepukika endapo tu watu watabadili tabia ya kupenda kufanya mazoezi .wewe mwananchi serikali yetu  kupitia kwa mama yetu mpendwa makamu wa raisi mama samia suluh imegundua kua watu wake wanaelekea kwenye  shimo. ikapelekea kuzindua siku maaalumu kwa ajili ya watu wote wafanye mazoezi .serikali ilizindua siku hiyo ili kukumbusha uwe na utamaduni wa kufanya mazoezi kwa faida ya kwako na jamii iliokuzunguka lakini cha ajabu watu wengi uzinduzi huu wanafananisha na uzinduzi wa barabara au uzinduzi mwingine kwani kiukweli bado watu hawajazinduka kabisa .unapomuambia mtu kuhusu mazoezi analeta visingizio vingi lakini sababu zote hizo hazina mashiko .kumbuka uzinduzi huu ni kuzindua akili yako ushike njia sahihi ya afya mwenye jukumu la kutunza afya ni jukumu la kila mtu mwenyewe binafsi wala sio jukumu la mama samia suluh wala sio la rais wetu magufuli.hakika kuumbwa kwetu hapa duniani ni kwa ajili ya kumtumikia mwenyezi mungu maana ya kumtumikia ni kufuata maagizo yake kwa hiyo mazoezi pia ni sehemu ya maagizo kwetu kutoka kwake kwani .mwili usipofanya mazoezi ni sawa na chuma kukaa bila kutumika lazime kishike kutu na kupelekea kuzeeka .hivyo ukishiriki mazoezi unategemea kupata faida mbili kwa wakati mmoja kwanza utapata Baraka  kwa sababu umetekeleza kanuni alizotuwekea .na faida ya pili utaboresha afya yako.pia usipofanya mazoezi unapata hasara mbili kwa wakati mmoja kwanza utapata dhambi kwa kua umekataa maamrisho ya mwenyezi mungu pia utapata afya mbovu na ukipoteza maisha chanzo chake kikibainika kwa sababu ya kutofanya mazoezi bila shaka hautakua tofauti na mtu aliepoteza maisha kwa kujinyonga kwani Yule aliejinyonga kwa kamba katumia maamuzi ya ghafla lakini mtu aliekufa kwa maradhi nyemelezi amejinyonga taratibu kwa muda mrefu.kwa hiyo acha kufuata kamba utakayotumia kujinyonga kwa kufuata njia sahihi ya afya NAMALIZIA KUSEMA ZINDUKA……ZINDUKA……ZINDUKA…….MAMA SAMIA  SULUH  AMEKUZINDUA