Manchester City wataweza kulipa kisasi kwa Liverpool UEFA leo? - MALIKITA SAFARI FITNESS

Recent Posts

test

Tuesday 10 April 2018

Manchester City wataweza kulipa kisasi kwa Liverpool UEFA leo?


Ni katika mchezo wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya ambapo kwa hakika Man City wana kibarua kizito sana kwani wanatakiwa kuifunga Liverpool bao 4-0 maana mechi iliyopita, Man City walibamizwa 3-0 pale Anfield mjini Liverpool.
Wachezaji wa Timu ya Man City wakishangilia goli lililofungwa na Mchezaji Sergio Kun Aguero hivi karibuni.
Kiungo wa City, Fernandinho mwenye umri wa miaka 32 anasema lile juma gumu lililowakabili la kuchapwa kila walikoenda sasa limeisha na ni wakati sasa wa wachezaji wazoefu kuchukua nafasi yao na kuliongoza Jahazi.
Tangu Man City walipopoteza pale Anfield jumatano, pia katika ligi walichapwa 3-2 na Manchester United.
Liverpool ilifunga mara tatu ndani ya dakika 19 za kipindi cha kwanza katika mzunguko wa kwanza.
Ikiwa upande wa Jurgen Klopp utaweza kushinda katika Uwanja wa Etihad, City watalazimika kushinda angalau mara tano ili kuendelea kufikia nafasi ya nne.
Ni Timu mbili pekee katika historia ya Champions League ambazo zimewahi kujikwamua kutoka katika deni la magoli matatu au Zaidi katika kipindi cha mtoano. Sawa na deni analokabiliana nalo Man City.
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia mojawapo ya magoli waliyoyafunga msimu huu, 2018
Deportivo La Coruna ikiwa nyuma ya AC Milan 4-1 mwaka 2004 walifanikiwa kupindua matokeo kwa 4-0 in katika mechi ya marudiano.
Katika siku za hivi karibuni, ni Barcelona iliyobadilisha matokeo ya 4-0 dhidi ya Paris St-Germain kwa kushinda 6-1 katika mechi ya marudio uwanja wa Noe Camp msimu uliopita.
Katika mchezo mwingine wa marudiano robo fainali ya mabingwa Ulaya, Roma itashuhudiwa wakikwaana na Barcelona katika uwanja wa Stadio Olimpico.
Nyota wa klabu ya soka ya Barcelona Luis Suarez, Lionel Messi na Moussa Dembele wakishangilia goli waliloifungia klabu hiyo hivi karibuni.
Meneja wa Roma Eusebio di Francesco amekiri kwamba kwa hakika kukutana na Barcelona anakutana na alichokiita Mashine lakini anabaki na matumaini makubwa.
Waitaliano hao wanakutana na Wahispania huku waitaliano wakiwa na hasira za kuchapwa bao 4-1 katika mzunguko wa kwanza.
Pia Roma walichapwa 2-0 na Fiorentina aliyeko nafasi ya saba na sasa wana point 21 nyuma ya viongozi wa Seria A Juventus
Wachezaji wa AS Roma kwenye moja ya michezo yao ya hivi karibuni kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa ya Ulaya, 2018
Katika hali ya tofauti, Barcelona wakiwa na Lionell Messi wako pointi 11 juu na bado Meneja wao Ernesto Valverde pamoja na kuwa watakuja na faida ya magoli matatu kibindoni bado amesema mechi hii dhidi ya Roma hawataichukulia kawaida na kwa hakika wataingia Uwanjani kama vile matokeo ni 0-0.
Katika upande wa Championship Cardiff City wataondoka katika nafasi ya pili kama watashindwa kuwapiga Aston Villa na iwapo pia Fulham itawachapa Reading wanaopambana kujiokoa kushuka daraja.
Source: BBC