Leo
tutazungumzia kuhusu urembo au muonekano(shape)
Kila mtu
anapenda aonekane mzuri machoni mwa jamii iliomzunguka.uzuri ni maana pana au
ina mambo mengi sana ila nitaelezea kwa
uchache tu kama vile uzuri wa ngozi na muonekano wa umbo (shape).Bila shaka
unaweza kua shahidi kwa namna moja ama nyingine tunashudia serikali yetu
pendwa ikitumia nguvu kubwa kukataza na
kupiga vita wananchi wake wasitumie vipodozi
na madawa mengine yenye viambata vyenye sumu kwa lengo la kutaka
urembo.ila kwa bahati mbaya pamoja na kutumia nguvu kubwa lakini bado wananchi
walengwa hawaoni au kutii amri ya serikali kuacha kutumia bidhaa hizo.japo
serikali imewalenga zaidi wafanya biashara wanaouza bidhaa hizo.wakati walengwa
wakiendelea kutafuta bidhaa hizo kwa hali na gharama yeyote ile ili watumiekama
nilivyosema kila mmoja anatamani urembo
kwa hiyo watu walio wengi wanapenda
matokeo ya haraka bila kujali kama njia wanayoitumia ni sahihi au la.kwa kifupi
watu wanapenda kutumia njia ya
mkato.mwenyezi mungu ametuumba tofauti tofauti kwa maksudi yake wala hajafanya
makosa katika hilo.ninamaanisha kuwa kuna
wanene,wembamba,wafupi,warefu,weupe,weusi,maji ya kunde nk.sawa na hali nilizorodhesha
hapo juu kila mmoja ajijue yupo kwenye kundi gani. hatmae usimame kwenye kioo
na ujiangalie hatmae umshukuru sana mwenyezi mungu na kumpa sifa lukuki kwa
kukuumba hivyo ulivyo ikiwezekana piga na vigele gele kuonyesha
furaha yako. Kwani wewe hivyo ulivyo ni mrembo na mzuri endapo tu utafuata njia
sahihi na salama .ila kinyume chake watu walio wengi wanajichukia na
kutokujikubali kujiona hivyo walivyo na kutamani shape na rangi ya watu wengine.
na kupelekea kutumia gharama kubwa kwa kununua vipodozi au madawa yenye viambata vyenye sumu
na kuharibu afya zao.mwili wa mwanadamu sio sawa na chuma unataratibu zake
namna ya kuufanya uwe na muonekano mzuri kuanzia (shape)umbo,ngozi .nk .chuma
unaweza ukakiokota vichakani ukaamua kionekane kipya kwa kupaka rangi .wakati
mwili ili ngozi ionekane vizuri inanzia ndani ya mwili hadi nje ya mwili walio
wengi wanakazania muonekano wa nje tu
bila kuanzia ndani .njia ya kua na muonekano mzuri ni rahisi sana wala haina
gharama ni kufanya mazoezi ya viungo tu.kwani unapofanya mazoezi faida yake ni
kubwa na nyingi japo leo tunazungumzia
kuhusu urembo tu.
MAZOEZI YANA
FANYAJE KAZI KWENYE UREMBO WA NGOZI?
Mazoezi
yanasaidia sana kwenye urembo wa ngozi .kwani unapofanya mazoezi na kutoa jasho inafungua vinyweleo au vitundu
vidogo vilivyo kwenye ngozi na kupelekea kusaidia ngozi kua katika muonekano
mzuri,sababu ya pili utahitaji kunywa maji mengi kwani unaposhiriki mazoezi hupelekea kua na
uhitaji mkubwa wa maji (KIU)na unapokunywa maji mengi inasaidia kua na afya ya
ngozi,sababu ya tatu ni kwamba mwenyezi mungu ametupatia aina nyingi ya chakula
na kila chakula kina fanya kazi yake katika mwili wa mwanadamu .unapofanya
mazoezi husaidia kuharakisha mwendo wa chakula ambacho kimepangwa kifanye kazi
katika eneo la ngozi.sababu zipo nyingi ila kwa hizo chache nilizozitaja
inaonyesha picha kiasi gani umuhimu wa mazoezi kwa watu wote wanawake kwa
wanaume
MAZOEZI YANAFANYAJE
KAZI KUTENGENEZA UMBO(SHAPE)
Mazoezi
yanafanya kazi moja ambayo naweza kuiiita ya ajabu sana.kwani yanaongeza mwili
lakini pia yanapunguza mwili kwa wakati mmoja kutegemeana na mtu alivyo yaani
ni mnene au mwembamba.kwa kifupi yanamuacha mtu asili alionayo
Mfano;kama mtu
asili yake ni mnene alafu hafanyi mazoezi
atakua mnene zaidi .akishiriki mazoezi mara kwa mara itapunguza ziada
aliyonayo atabaki na unene wa asili yake na kupelekea kua mwepesi na ukakamavu
na kuongeza nguvu nk.hivyo hawezi kujichukia mwenyewe kwani sisi wote ni
mashahidi mtu akiwa mnene hua
anaitwa majina mengi yenye kuudhi na yasiofaa kama vile huitwa minyama uzembe,bonge,na mengi mengineyo yasiyofaa
kuandikwa .kwa hiyo majina ya hovyo anayoitwa ukijumlisha na udhaifu alionao
hupelekea kujichukia na kutamani umbo la mtu
mwingine na kulaani alivyo
Mfano
mwingine;kama mtu ni mwembamba halafu hauna kawaida ya kushiriki mazoezi unakua
mwembamba zaidi .ukishiriki mazoezi mara kwa mara unaongezeka mwili(unene) japo
huwezi kunenepa kufikia hatua ya kuonekana bonge. Kwa hiyo hutoitwa tena majina
ya hovyo na ya kuudhi kama vile mchongoma,kimbaumbau nk.na kupelekea
kuijichukia na kulaani umbile ulilonalo .fanya mazoezi uwe na umbo (SHAPE) ya
kuvutia pia upate na faida zingine za
afya.ZINDUKA…..ZINDUKA…..ZINDUKA…… MAMA SAMIA SULUHU AMEKUZINDUA